Tanzanian 4-H GKC
Dhana ya Kituo cha Maarifa cha Kimataifa 4H (GKC) ni kusaidia vikundi nchini Tanzania na duniani kote kutumia mtindo wa 4-H kama mfano wa kujenga maisha endelevu na kuboresha usalama wa kiuchumi kwa vijana. Kituo hiki kinatoa rasilimali na zana za kujenga jamii, na kusaidia vijana wa Tanzania kuianzisha miradi ya kilimo, kutafuta majibu ya matatizo yaliyoibuliwa, na kuendeleza ujuzi wao kiuongozi.
Kwenye tovuti hii, utapata zana za kimtandao ambazo zinatoa
- Nyenzo za kujifunza—misaada ya kiufundi ambayo inaboresha utendaji katika kilimo na maendeleo ya vijana
- Mabaraza ya jamii—Huu ni mtandao unaoweza kuunganisha vilabu vyote vya 4H hapa Tanzania na kwingineko kote duniani
- Muulize mtaalamu—uliza swali na utaweza kupata jibu linalohusiana zaidi na utamaduni wa sehemu husika
Kwa habari zaidi kuhusu 4-H Tanzania, tafadhali tembelea tovuti yao.
Translated by Ibrahim Yusuf, Project Office, Tanzania 4H Organization, Tanga.
